Skip to main content

Kairo Yaliyomo Jiografia | Kanda ya Jiji | Dini | Tazama pia | Marejeo | Viungo vya nje | Urambazaji30°03′N 31°22′E / 30.05°N 31.367°E / 30.05; 31.367www.cairo.gov.egAl-Qāhirah (Governorate) 2011Wakazi wa Kairo KubwaCairo Mapsya awaliEgypt: Governorates & CitiesTen Facts about Cairo, EgyptBiblical snowstorm: Rare flakes in Cairo, Jerusalem paralyzed by over a footEgypt unveils plans to build new capital east of CairoTravel CairoAl-Ahram Weekly | Features | Reaching an impasseya awaliTovuti rasmiÉgypte : 24 coptes tués par les forces de l'ordre au Caire – Le PointCairoTovuti rasmiCairokuihariri na kuongeza habari

Pages using ISBN magic linksMbegu za jiografia ya AfrikaMiji Mikuu AfrikaMisriMiji ya MisriNileKairo


Kiarabumji mkuuMisrimjimajijidunianikaskaziniMisrikilomitakusinipwanibahariMediteraneamto Nilebondejangwadeltakm2masharikivisiwakarne ya 19handakimiferejiHistoriaGarden CityKairo mjiniZamalekKairo ya KaleBabyloni ya MisriBizantiuvamiziWaarabuWaislamuFustatBulaqbandarikarne ya 16Bomaar.WafatimibarabaranyumbatabianchinusutropikiyabisihewaunyevuHalijotowastanisentigredimvuamilimitaMwezijotoJulaiJanuariUsimbishajiNovembaMachi2013thelujiKanda ya JijiIdadimilionimkoa wa KairomikoaGizaQalyubiaUsafirikanda ya jijinjia za relireli ya chini ya ardhiferimagariteksimabasiummaMetro ya KairoardhiMabehewasaakaziniwanawakeurefutramuHeliopolismji wa NasrduaraMadarajatamadunidininyumba zao za ibadahistoriaWagiriki wa Misrimapinduzi1952Wayahudiubaguzivita ya Israeli na Waarabu wa 1948WaislamuWasunni%WakristoWakoptimisikitiChuo Kikuu cha Al-Azhar969taasisiutalaamukiongoziPapa Pope Tawadros IIKanisa la Mtakatifu Marko mjini KairokanisabaraAfrikaMasingagogiwataliiibadaitikadi kali












Kairo




Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru






Jump to navigation
Jump to search









Kairo

Kitovu cha mji wa Kairo

Kitovu cha mji wa Kairo



Bendera

Majiranukta: 30°03′N 31°22′E / 30.05°N 31.367°E / 30.05; 31.367

Nchi

Misri

Mkoa

Kairo

Tovuti: www.cairo.gov.eg



Kairo jinsi inavyoonekana kutoka angani - njano ni rangi ya jangwa, kijani-nyeusi ni rangi ya mashamba kwenye bonde la Nile linalopanuka kuwa delta na rangi ya kijivu ni nyumba za Kairo


Kairo (kwa Kiarabu القاهرة al-Qāhira – „mwenye ushindi“) ni mji mkuu wa Misri na mji mkubwa wa nchi zote za Kiarabu, pia moja kati ya majiji makubwa duniani.


Kairo yenyewe inakadiriwa kuwa na wakazi 10,230,350 [1], kanda ya jiji pamoja na mitaa ya nje na mapembizo ni 15,628,325 [2].




Yaliyomo





  • 1 Jiografia

    • 1.1 Tabianchi ya Kairo



  • 2 Kanda ya Jiji

    • 2.1 Usafiri



  • 3 Dini


  • 4 Tazama pia


  • 5 Marejeo


  • 6 Viungo vya nje




Jiografia |




Sehemu ya kusini ya kisiwa cha Gezira kilichopo ndani ya mto Nile, Opera ya Kairo (jengo jeupe) na nyuma kitovu cha mji pamoja na meidani ya Tahrir ng'ambo ya mto.




Mto Nile unapita mjini Kairo.




Kisiwa cha Gezira katikati ya jiji.


Kairo iko kwenye sehemu ya kaskazini ya Misri, takriban kilomita 160 kusini kwa pwani ya bahari ya Mediteranea. Mji ulikua kando ya mto Nile, mahali ambako unatoka katika bonde unamovuka jangwa na kujigawa kuwa na delta pana hadi baharini.


Jinsi ilivyo kwenye majiji mengi makubwa, wenyeji hutofautisha kati ya mji asilia wenyewe na jiji kubwa kwa jumla. Mji wa Kairo wenyewe una eneo la km2 453 tu, uko upande wa mashariki wa mto pamoja na visiwa viwili ndani ya mto; jiji pamoja na vitongoji limepanuka pande zote mbili kuelekea ndani ya jangwa.[3][4]


Katika karne ya 19 mto Nile ulibanwa na handaki na mifereji. Hadi wakati ule mifuriko na mabadiliko kwenye mwendo wake walitokea mara kwa mara. Historia hii ya mabadilko ya mwendo wa mto ni sababu ya kwamba mitaa mipya ya mji iko karibu na mto wenyewe mahali ambako zamani wangeogopa kujenga, ni mitaa ya Garden City, Kairo mjini na Zamalek.[5]


Kusini mwa Kairo ya leo kuna Kairo ya Kale penye mabaki ya miji iliyotangulia hapa kama vile Babyloni ya Misri (enzi ya Bizanti, kabla ya uvamizi wa Waarabu Waislamu) na Fustat (mji mkuu wa kwanza wa Kiislamu nchini Misri).


Sehemu za Bulaq ziko leo upande wa kaskazini ya mji wenyewe zilianzishwa kama eneo la bandari ya mtoni mnamo karne ya 16. Boma la Kairo (ar. qale salah ad din) inaonyesha mahali ambako mji wa Kairo ulianzishwa na Wafatimi. Upande wa magharibi wa mji wa Kairo uliathiriwa na mpangilio wa jiji wa kimagharibi ukiwa na barabara pana, nyanja mbalimbali na nyumba za kisasa. Upande wa mashariki una zaidi mitaa midogomidogo, nyumba za kienyeji na kujaa watu wengi mno.



Tabianchi ya Kairo |


Kairo iko katika kanda yenye tabianchi ya nusutropiki. Tabianchi kwa jumla ni yabisi. Hata hivyo wakati mwingine hewa yenye unyevu inaweza kufika kwa sababu bahari iko karibu. Halijoto ya wastani mwakani ni sentigredi 21.7. Kiwango cha mvua ni milimita 24,7 pekee. Mwezi wenye joto zaidi ni Julai mwenye wastani wa sentigredi 28, na mwezi baridi ni Januari yenye wastani wa sentigredi 13,9.


Usimbishaji ni mdogo; wastani wa mwaka ni milimita 24,7 pekee unaotiririka katika miezi wa Novemba hadi Machi pekee.


Wakati wa Disemba 2013 Kairo iliona theluji mara ya kwanza baada ya miaka mingi sana[6].



Kanda ya Jiji |


Kanda ya Jiji inajumlisha Kairo pamoja na miji jirani, vitongoji na mapembizo. Idadi ya wakazi kwa jumla iko kati ya milioni 15 hadi 16. Kiutawala kanda ya jiji inajumlisha mkoa wa Kairo na sehemu ya mikoa miwili yaani Giza na Qalyubia.


Miji ya pekee muhimu zaidi katika kanda hii ni


  • Kairo

  • Giza


  • Helwan, pamoja Mji wa 15 Mei

  • Shubra El-Kheima

  • Mji wa 6 Oktoba

  • Mji wa Badr

  • Kairo mpya

  • Heliopolis Mpya

  • Mji wa Basus

Kuna mipango ya kujenga jiji jipya upande wa mashariki wa Kairo litakalokuwa mji mkuu mpya wa Misri.[7]



Usafiri |





Metro ya Kairo




Barabara Kuu mjini




Mabasi ya manispaa




Kituo cha Metro Ramses


Usafiri ndani ya Kairo na kanda ya jiji huenda kwa kutumia barabara, njia za reli, reli ya chini ya ardhi inayoitwa "metro" na feri kwenye mto. Kuna magari mengi ya binafsi, teksi na mabasi ambayo ni ya umma au ya binafsi. Njia nyingi za mabasi na reli ya metro zinakutana kwenye Midan Ramses [8]
Usafiri ndani ya Kairo ni mashuhuri kwa ugumu wake kutokana na wingi wa watu na magari.[9]




Ramani ya Metro ya Kairo


Metro ya Kairo ("مترو") ni jina la reli ya chini ya ardhi. Ni usafiri wa haraka pale njia zake zinapofika. Mabehewa yake yanaweza kujaa mno wakati wa saa za kwenda kazini na kurudi. Kila treni ya metro huwa na magari wawili yaliyotengwa kwa ajili ya wanawake pekee, ni gari la nne na la tano, lakini hata hivyo wakinamama wako huru kupanda kila behewa wanapotaka. Metro hii ina njia tatu zenye urefu wa kilomita 77.9 na kuna vituo 61 zinazohudumiwa[10].


Kuna tramu katika sehemu za (Heliopolis na mji wa Nasr) lakini ile katika Kairo mjini ilifungwa miaka mingi iliyopita.


Kuna mtandao mkubwa wa barabara kati ya Kairo mjii, sehemu nyngine za kanda ya jiji na miji ya nje. Kuna barabara ya duara inayopita nje ya jiji. Madaraja mengi yanalenga kurahisisha mwendo ndani ya jiji ingawa kwenye saa za msongamano watu hukaa sana kwenye foleni za magari.



Dini |


Zamani Kairo ilikuwa mji wenye wakazi wengi wa tamaduni na dini mbalimbali; hadi leo nyumba zao za ibada ni kama kumbukubu ya historia hiyo. Maelfu ya Wagiriki wa Misri waliondoka nchini baada ya mapinduzi ya mwaka 1952. Wayahudi pia walianza kuona ubaguzi mkali na madhulumu tangu vita ya Israeli na Waarabu wa 1948 wakaondoka. Leo hii kuna Wayahudi chini ya 100 waliobaki Misri baada ya historia ya miaka 2,500.


Siku hizi wakazi walio wengi ni Waislamu Wasunni (takriban 90%). Wengine ni hasa Wakristo Wakopti.


Upande wa Uislamu kuna misikiti mingi na idadi yake inaendelea kuongezeka. Chuo Kikuu cha Al-Azhar kinapatikana mjini tangu mwaka 969: ni taasisi ambayo utalaamu wake unaheshimiwa na kuangaliwa kati wa Wasunni wengi duniani.


Upande wa Wakopti kiongozi wao Papa Pope Tawadros II anakaa Kairo. Kanisa la Mtakatifu Marko mjini Kairo ni kanisa kubwa la pili kwenye bara la Afrika.


Masingagogi ya Kiyahudi yanaweza kutembelewa na watalii lakini hakuna tena ibada ya kawaida kutokana na idadi ndogo ya Wayahudi waliobaki.


Vurugu za kisiasa za miaka iliyopita ilileta pia magongano kati ya wafuasi wa dini, hasa kati ya Waislamu wenye itikadi kali na Wakristo. [11]



Tazama pia |



  • Piramidi za Giza ziko karibu na Kairo

  • Orodha ya miji ya Misri


Marejeo |



  1. Walikuwa 7,902,085 mwaka 2011 wakati wa sensa, taz. Al-Qāhirah (Governorate) 2011


  2. Wakazi wa Kairo Kubwa walihesabiwa katika sensa ya 2011 kuwa 15,628,325.


  3. Cairo Maps. Cairo Governorate. Jalada kutoka ya awali juu ya 19 April 2009. Iliwekwa mnamo 10 September 2009.


  4. Brinkhoff, Thomas. Egypt: Governorates & Cities. City Population. Iliwekwa mnamo 12 September 2009.



  5. Amanda Briney (20 February 2011). Ten Facts about Cairo, Egypt. Geography of Cairo. About.com. Iliwekwa mnamo 14 July 2012.



  6. Samenow, Jason (13 December 2013). "Biblical snowstorm: Rare flakes in Cairo, Jerusalem paralyzed by over a foot". The Washington Post.


  7. "Egypt unveils plans to build new capital east of Cairo". BBC News. 13 March 2015. Retrieved 14 March 2015.


  8. (2007) Travel Cairo. MobileReference. ISBN 978-1-60501-055-7. 


  9. Al-Ahram Weekly | Features | Reaching an impasse. Weekly.ahram.org.eg (1 February 2006). Jalada kutoka ya awali juu ya 18 May 2009. Iliwekwa mnamo 5 May 2009.


  10. Tovuti rasmi


  11. Égypte : 24 coptes tués par les forces de l'ordre au Caire – Le Point. Lepoint.fr. Iliwekwa mnamo 12 March 2013.


Viungo vya nje |



WikiMedia Commons


Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Cairo



  • Tovuti rasmi

  • Cairo




Africa satellite plane.jpg
Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Kairo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.



Rudishwa kutoka "https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Kairo&oldid=1058543"










Urambazaji


























(window.RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgPageParseReport":"limitreport":"cputime":"0.156","walltime":"0.203","ppvisitednodes":"value":1568,"limit":1000000,"ppgeneratednodes":"value":0,"limit":1500000,"postexpandincludesize":"value":16253,"limit":2097152,"templateargumentsize":"value":6095,"limit":2097152,"expansiondepth":"value":22,"limit":40,"expensivefunctioncount":"value":1,"limit":500,"unstrip-depth":"value":0,"limit":20,"unstrip-size":"value":6386,"limit":5000000,"entityaccesscount":"value":0,"limit":400,"timingprofile":["100.00% 125.769 1 -total"," 58.20% 73.194 1 Kigezo:Infobox_Settlement"," 27.53% 34.627 1 Kigezo:Geobox_coor"," 24.48% 30.791 1 Kigezo:Coord"," 20.35% 25.592 1 Kigezo:Coord/display/inline"," 17.59% 22.123 1 Kigezo:Coord/input/dm"," 14.75% 18.550 1 Kigezo:Coord/link"," 9.13% 11.487 2 Kigezo:Coord/dms2dec"," 6.84% 8.607 5 Kigezo:Cite_web"," 6.61% 8.316 2 Kigezo:Precision1"],"cachereport":"origin":"mw1303","timestamp":"20190417084352","ttl":2592000,"transientcontent":false););"@context":"https://schema.org","@type":"Article","name":"Kairo","url":"https://sw.wikipedia.org/wiki/Kairo","sameAs":"http://www.wikidata.org/entity/Q85","mainEntity":"http://www.wikidata.org/entity/Q85","author":"@type":"Organization","name":"Uchangiaji katika miradi ya Wikimedia","publisher":"@type":"Organization","name":"Wikimedia Foundation, Inc.","logo":"@type":"ImageObject","url":"https://www.wikimedia.org/static/images/wmf-hor-googpub.png","datePublished":"2006-06-20T12:17:38Z","dateModified":"2019-03-18T14:49:46Z","image":"https://upload.wikimedia.org/wikipedia/commons/3/3b/Kairo_001.jpg","headline":"mji mkuu wa Misri"(window.RLQ=window.RLQ||[]).push(function()mw.config.set("wgBackendResponseTime":138,"wgHostname":"mw1267"););

Popular posts from this blog

19. јануар Садржај Догађаји Рођења Смрти Празници и дани сећања Види још Референце Мени за навигацијуу

Israel Cuprins Etimologie | Istorie | Geografie | Politică | Demografie | Educație | Economie | Cultură | Note explicative | Note bibliografice | Bibliografie | Legături externe | Meniu de navigaresite web oficialfacebooktweeterGoogle+Instagramcanal YouTubeInstagramtextmodificaremodificarewww.technion.ac.ilnew.huji.ac.ilwww.weizmann.ac.ilwww1.biu.ac.ilenglish.tau.ac.ilwww.haifa.ac.ilin.bgu.ac.ilwww.openu.ac.ilwww.ariel.ac.ilCIA FactbookHarta Israelului"Negotiating Jerusalem," Palestine–Israel JournalThe Schizoid Nature of Modern Hebrew: A Slavic Language in Search of a Semitic Past„Arabic in Israel: an official language and a cultural bridge”„Latest Population Statistics for Israel”„Israel Population”„Tables”„Report for Selected Countries and Subjects”Human Development Report 2016: Human Development for Everyone„Distribution of family income - Gini index”The World FactbookJerusalem Law„Israel”„Israel”„Zionist Leaders: David Ben-Gurion 1886–1973”„The status of Jerusalem”„Analysis: Kadima's big plans”„Israel's Hard-Learned Lessons”„The Legacy of Undefined Borders, Tel Aviv Notes No. 40, 5 iunie 2002”„Israel Journal: A Land Without Borders”„Population”„Israel closes decade with population of 7.5 million”Time Series-DataBank„Selected Statistics on Jerusalem Day 2007 (Hebrew)”Golan belongs to Syria, Druze protestGlobal Survey 2006: Middle East Progress Amid Global Gains in FreedomWHO: Life expectancy in Israel among highest in the worldInternational Monetary Fund, World Economic Outlook Database, April 2011: Nominal GDP list of countries. Data for the year 2010.„Israel's accession to the OECD”Popular Opinion„On the Move”Hosea 12:5„Walking the Bible Timeline”„Palestine: History”„Return to Zion”An invention called 'the Jewish people' – Haaretz – Israel NewsoriginalJewish and Non-Jewish Population of Palestine-Israel (1517–2004)ImmigrationJewishvirtuallibrary.orgChapter One: The Heralders of Zionism„The birth of modern Israel: A scrap of paper that changed history”„League of Nations: The Mandate for Palestine, 24 iulie 1922”The Population of Palestine Prior to 1948originalBackground Paper No. 47 (ST/DPI/SER.A/47)History: Foreign DominationTwo Hundred and Seventh Plenary Meeting„Israel (Labor Zionism)”Population, by Religion and Population GroupThe Suez CrisisAdolf EichmannJustice Ministry Reply to Amnesty International Report„The Interregnum”Israel Ministry of Foreign Affairs – The Palestinian National Covenant- July 1968Research on terrorism: trends, achievements & failuresThe Routledge Atlas of the Arab–Israeli conflict: The Complete History of the Struggle and the Efforts to Resolve It"George Habash, Palestinian Terrorism Tactician, Dies at 82."„1973: Arab states attack Israeli forces”Agranat Commission„Has Israel Annexed East Jerusalem?”original„After 4 Years, Intifada Still Smolders”From the End of the Cold War to 2001originalThe Oslo Accords, 1993Israel-PLO Recognition – Exchange of Letters between PM Rabin and Chairman Arafat – Sept 9- 1993Foundation for Middle East PeaceSources of Population Growth: Total Israeli Population and Settler Population, 1991–2003original„Israel marks Rabin assassination”The Wye River Memorandumoriginal„West Bank barrier route disputed, Israeli missile kills 2”"Permanent Ceasefire to Be Based on Creation Of Buffer Zone Free of Armed Personnel Other than UN, Lebanese Forces"„Hezbollah kills 8 soldiers, kidnaps two in offensive on northern border”„Olmert confirms peace talks with Syria”„Battleground Gaza: Israeli ground forces invade the strip”„IDF begins Gaza troop withdrawal, hours after ending 3-week offensive”„THE LAND: Geography and Climate”„Area of districts, sub-districts, natural regions and lakes”„Israel - Geography”„Makhteshim Country”Israel and the Palestinian Territories„Makhtesh Ramon”„The Living Dead Sea”„Temperatures reach record high in Pakistan”„Climate Extremes In Israel”Israel in figures„Deuteronom”„JNF: 240 million trees planted since 1901”„Vegetation of Israel and Neighboring Countries”Environmental Law in Israel„Executive branch”„Israel's election process explained”„The Electoral System in Israel”„Constitution for Israel”„All 120 incoming Knesset members”„Statul ISRAEL”„The Judiciary: The Court System”„Israel's high court unique in region”„Israel and the International Criminal Court: A Legal Battlefield”„Localities and population, by population group, district, sub-district and natural region”„Israel: Districts, Major Cities, Urban Localities & Metropolitan Areas”„Israel-Egypt Relations: Background & Overview of Peace Treaty”„Solana to Haaretz: New Rules of War Needed for Age of Terror”„Israel's Announcement Regarding Settlements”„United Nations Security Council Resolution 497”„Security Council resolution 478 (1980) on the status of Jerusalem”„Arabs will ask U.N. to seek razing of Israeli wall”„Olmert: Willing to trade land for peace”„Mapping Peace between Syria and Israel”„Egypt: Israel must accept the land-for-peace formula”„Israel: Age structure from 2005 to 2015”„Global, regional, and national disability-adjusted life years (DALYs) for 306 diseases and injuries and healthy life expectancy (HALE) for 188 countries, 1990–2013: quantifying the epidemiological transition”10.1016/S0140-6736(15)61340-X„World Health Statistics 2014”„Life expectancy for Israeli men world's 4th highest”„Family Structure and Well-Being Across Israel's Diverse Population”„Fertility among Jewish and Muslim Women in Israel, by Level of Religiosity, 1979-2009”„Israel leaders in birth rate, but poverty major challenge”„Ethnic Groups”„Israel's population: Over 8.5 million”„Israel - Ethnic groups”„Jews, by country of origin and age”„Minority Communities in Israel: Background & Overview”„Israel”„Language in Israel”„Selected Data from the 2011 Social Survey on Mastery of the Hebrew Language and Usage of Languages”„Religions”„5 facts about Israeli Druze, a unique religious and ethnic group”„Israël”Israel Country Study Guide„Haredi city in Negev – blessing or curse?”„New town Harish harbors hopes of being more than another Pleasantville”„List of localities, in alphabetical order”„Muncitorii români, doriți în Israel”„Prietenia româno-israeliană la nevoie se cunoaște”„The Higher Education System in Israel”„Middle East”„Academic Ranking of World Universities 2016”„Israel”„Israel”„Jewish Nobel Prize Winners”„All Nobel Prizes in Literature”„All Nobel Peace Prizes”„All Prizes in Economic Sciences”„All Nobel Prizes in Chemistry”„List of Fields Medallists”„Sakharov Prize”„Țara care și-a sfidat "destinul" și se bate umăr la umăr cu Silicon Valley”„Apple's R&D center in Israel grew to about 800 employees”„Tim Cook: Apple's Herzliya R&D center second-largest in world”„Lecții de economie de la Israel”„Land use”Israel Investment and Business GuideA Country Study: IsraelCentral Bureau of StatisticsFlorin Diaconu, „Kadima: Flexibilitate și pragmatism, dar nici un compromis în chestiuni vitale", în Revista Institutului Diplomatic Român, anul I, numărul I, semestrul I, 2006, pp. 71-72Florin Diaconu, „Likud: Dreapta israeliană constant opusă retrocedării teritoriilor cureite prin luptă în 1967", în Revista Institutului Diplomatic Român, anul I, numărul I, semestrul I, 2006, pp. 73-74MassadaIsraelul a crescut in 50 de ani cât alte state intr-un mileniuIsrael Government PortalIsraelIsraelIsraelmmmmmXX451232cb118646298(data)4027808-634110000 0004 0372 0767n7900328503691455-bb46-37e3-91d2-cb064a35ffcc1003570400564274ge1294033523775214929302638955X146498911146498911

Кастелфранко ди Сопра Становништво Референце Спољашње везе Мени за навигацију43°37′18″ СГШ; 11°33′32″ ИГД / 43.62156° СГШ; 11.55885° ИГД / 43.62156; 11.5588543°37′18″ СГШ; 11°33′32″ ИГД / 43.62156° СГШ; 11.55885° ИГД / 43.62156; 11.558853179688„The GeoNames geographical database”„Istituto Nazionale di Statistica”проширитиууWorldCat156923403n850174324558639-1cb14643287r(подаци)